• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe za Watumishi |
Ilala Municipal Council
Ilala Municipal Council

The United Republic of Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Manispaa ya Ilala

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Core Values
    • Council Strategies
    • Mawasiliano
      • Wakuu wa Idara na Vitengo
      • Watendaji wa Kata
      • Maafisa Tarafa
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Administration and Personnel
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maji
      • Agriculture, irrigation and Coperative
      • Livestock and Fisheries Development
      • Land and Planning
      • Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
      • Ujenzi
      • Solid Waste Management and Environmental Conservation
    • Units
      • Legal
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Information Technology and Communication
      • Ugavi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuki
    • Administration Area
  • Fursa na Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
      • Historical Buildings
      • Landmarks
      • Museums and Art Galleries
      • Seafront Development
      • Libraries and Cultural Centers
    • Kilimo
    • Business and Marketing
    • Housing Area
    • Bus Stand
  • Huduma
    • Elimu
    • Afya
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo na Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
    • Huduma za Kifedha
    • Masoko
    • Usafirishaji
  • Madiwani
    • All Councilors
    • Council Committee
      • Town Planning and Environmental
      • Finance and Administration
      • Economical and Social Welfare
      • Kamati ya UKIMWI
      • Kamati ndogo za Halmashauri
    • Council Meetings
    • Mayor's Timetable
    • Orodha ya Mameya
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi iliyo kwenye Mpango
    • Miradi inayoendelea
  • Machapisho
    • Sheria
    • By laws
    • Miongozo
    • Sera
    • Nyaraka
    • Fomu za Maombi
    • Ripoti
    • Taratibu
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Bajeti ya Manispaa
    • Mpango Mkakati
    • Socio-Economic Profile
    • Majarida
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Hotuba
  • Wilaya
    • Majukumu ya Ofisi ya Mkuu wa Wilaya

Elimu Msingi

Idara ya Elimu msingi ni moja kati ya idara kumi na tatu(13) zilizopo katika Halmashauri ya Manispaa ya Ilala. Muundo wa Idara ya Elimu msingi umegawanyika katika sehemu kuu tano (5) za kiutendaji ambazo ni;- Sehemu ya Taaluma, Sehemu ya Vifaa na Takwimu, Sehemu ya Elimu ya Watu wazima, Elimu Maalumu na  Sehemu ya Utamaduni. Kuwepo kwa vitengo hivi kumesaidia sana kuimarisha na uboresha utendaji kazi katika Idara ya Elimu Msingi.

 1.1      MALENGO NA MAJUKUMU YA IDARA YA ELIMU MSINGI 

Kazi kubwa ya Idara ya Elimu Msingi   ni kama ifuatavyo-:

  • Kuongeza uandikishaji kwa kuzingatia fursa sawa.
  • Kuinua ubora wa Elimu  katika ngazi zote kwa Halmashauri.
  • Kusimamia uwezo wa utendaji kazi.
  • Kushughulikia masuala ya mtambuka, kuimarisha taratibu za kitaasisi,
  • kufanya utafiti , ufuatiliaji na tathmini za kielimu.
  • Kupunguza idadi ya watu wazima wasiojua kusoma na kuandika
  • Kuinua ubora wa mazingira ya   Kufundishia na kujifunzia wanafunzi wote.
  • Kuongeza idadi ya madarasa na watoto wa shule za awali.
  • Kuhakikisha kuwa Elimu ya UKIMWI (VVU), Mazingira na stadi za maisha zinatolewa kwa ufanisi katika shule za msingi.
  • Kusimamia upatikanaji na uwezeshaji wa mazingira kwa wanafunzi wenye Ulemavu.
  • Kusimamia mapato na matumizi ya fedha  katika shule za Serikali.
  • Kuratibu uanzishwaji wa shule za Msingi
  • Kukusanya,kuchambua na kuunganisha Takwimu mbalimbali za shule (Awali,Msingi & EWW)
  • Kushughulikia maslahi ya Walimu na watumishi wasio walimu waliopo katika shule za Msingi kwenye Halmashauri.
  • Kusimamia na kufafanua sera na nyaraka mbalimbali za Elimu katika ngazi ya Halmashauri.

1.2 MIKAKATI ILIYOPO ILI KUBORESHA ELIMU NA KUINUA KIWANGO CHA TAALUMA.

  • Kuendelea kuhamasisha wananchi kuchangia miradi ya maendeleo yao wenyewe na kuondokana na fikra potofu za misaada kutoka nchi za wengine.
  • Kujenga shule za ghorofa katika maeneo madogo yanayopatikana hasa sehemu za mjini mfano maeneo ya kata za Minazimirefu, Vingunguti na Buguruni kupunguza msongamano kwa kushirikiana na wadau mbalimbali.
  • Kutekeleza shughuli muhimu kulingana na ufinyu wa bajeti uliopo.
  • Kuboresha Taaluma kwa kugawa maafisa Elimu kila kata kwa ajili ya ufuatiliaji wa karibu wa Taaluma na matatizo ya walimu.
  • Kuboresha miundo mbinu na mazingira ya kufundishia na kujifunzia kwa kutumia fursa zilizopo kwa kuzingatia Mpango wa Serikali wa utekelezaji wa  Elimu bila Malipo.
  • Kufanya vikao mbalimbali vya kila mwezi kati ya Maofisa Elimu, maafisa Elimu kata na Walimu Wakuu kwa kuzingatia ratiba maalum iliyoandaliwa.Vikao rasmi hufanyika mara moja kwa mwezi.
  • Uendeshaji wa Semina mbalimbali za masomo na semina za kitaalamu na kufanya mrejesho shuleni. Mfano: semina zimeshaanza kufanyika katika   kata Mpaka sasa wakishirikiana na Klasta.
  • Kuwajengea uwezo Kamati za Taaluma kwa kila shule ili kuweza kufanya upimaji na tathmini kupata mwelekeo wa Maendeleo ya Wanafunzi.
  • Kuimarisha Vyama (Clubs) za masomo,  K.K.K, na uazishwaji wa Klabu za Rushwa, madawa ya kulevya na lishe  shuleni.
  • Kushirikiana na wadau mbalimbali wa Elimu ili kuboresha mazingira ya ufundishaji na ujifunzaji. Mfano Wazazi, watu binafsi na mashirika mbalimbal na Makampuni

1.3.HALI HALISI YA ELIMU YA AWALI 

Halmashauri ya Manispaa ya Ilala ina jumla ya Shule/Vituo vya Elimu ya Awali 230 kati yake 118 ni vya Serikali na 112 visivyo vya serikali.Jumla ya wanafunzi kwa Elimu ya awali serikali ni 10,265 kati yake wavulana 5,224 na wasichana 5,041.kwa shule zisizo za Serikali wapo wavulana  3,566 na wasichana 3,363,hivyo kufanya jumla ya wanafunzi  kuwa 6,929.

1.4.HALI HALISI YA ELIMU YA MSINGI 

Halmashauri pia inazo jumla ya shule 230 za Msingi.Shule za Serikali zina jumla ya shule zipatazo 120  zenye jumla ya wanafunzi wapatao 176,680 kati yao wavulana 87,288  na wasichana 89,392 vilevile  kwa shule  110  zisizo za serikali zenye jumla ya wanafunzi  52404 miongoni mwao wavulana 25,643 na wasichana 26,761.

Jumla ya wanafunzi wote Awali na Msingi Serikali ni  186,945 kati  yao ni wavulana   ni 92,512,na wasichana ni 94,433 .

1.5.ELIMU MAALUMU 

Halmashauri  ina shule moja ya msingi ya wasichana ya kihistoria  Tanzania ambayo  inaitwa Uhuru Wasichana, yenye idadi ya wanafunzi wapatao 630  pamoja na shule mbili zinazotumia lugha ya kiingereza katika kufundisha na kujifunza,Sambamba na hilo Halmashauri inazo shule  13  za Wanafunzi wenye ulemavu zikiwemo shule mbili(2) za bweni za Buguruni Viziwi na Uhuru Mchanganyiko  na shule ,zingine za kutwa zenye vitengo.Jumla ya wanafunzi wapatao 949 kati yao wavulana 459 na wasichana 460. 

S/NA
SHULE
AINA YA WALEMAVU
WAV
WAS
JML
1.
Uhuru Mchanganyiko
Ulemavu wa Akili,Viziwi wasioona,na Wasioona
80
33
143
2.
Buguruni Viziwi
Viziwi na viziwi wasioona
100
154
254
3.
Airwing
Ulemavu wa Akili
25
50
75
4.
Mzambarauni
Viziwi
49
47
96
5.
Maarifa
Ulemavu wa Akili
37
35
72
6.
Mtendeni
Viziwi
21
26
47
7.
Tumaini
Ulemavu wa Akili
30
44
74
8.
Chanika
Ulemavu wa Akili
29
15
44
9.
Viwege
Ulemavu wa Akili
12
12
24
10.
Msimbazi Mseto
Usonji(Autism)
21
5
26
11.
Pugu Kajiungeni
Ulemavu wa Akili
43
23
66
12.
Yangeyange
Ulemavu wa Akili
8
4
12
13.
Kivule
Ulemavu wa Akili
4
12
16


Jumla kuu

459

460

949

 

 1.6.Shughuli za Elimu ya Watu Wazima 

Kitengo hiki kinatekeleza shughuli zifuatazo-: 

S/NA
                            PROGRAMU
IDADI YA VITUO
1.
Mpango wa Elimu ya Msingi kwa Waliokosa(MEMKWA
25
2.
Mpango wa Uwiano kati ya Elimu ya Watu Wazima na Jamii(MUKEJA)
12
3.
Program ya Elimu ya Sekondari Huria (PESH)
7
4.
Elimu Masafa na Ana kwa Ana(ODL)-
37
5.
Program ya Ndiyo Ninaweza (YES  I CAN)
13
6.
Mahabusu  ya Watoto
1
7.
Hospitali ya Muhimbili (Kitengo cha Saratani-Watoto)
1

 

 1.7. Sehemu ya Utamaduni

Kazi kubwa ya kitengo hiki ni kuhakikisha shughuli zote  za Sanaa,Michezo,Burudani mbalimbali ndani ya Manispaa ya Ilala zinakwenda salama.Aidha ,Usajili wa  Vilabu vya Michezo,na vikundi vya sanaa.Kusimamia matamasha na mashindano  mbalimbali ,sherehe za  kitaifa na Kimataifa.Pia kusimamia ukusanyaji wa mapato katika kumbi za burudani,matangazo,viwanja vya wazi ,usajili wa klabu  na kumbi za starehe.Wanasimamia michezo katika shule za msingi(UMITASHUMTA)  na uandaaji wa viwanja vya michezo.

Matangazo

  • MATOKEO YA MTIHANI WA DARASA LA SABA- MANISPAA YA ILALA ( M ) 2020 November 21, 2020
  • MATOKEO YA MTIHANI WA DARASA LA SABA- MANISPAA YA ILALA ( V ) 2020 November 21, 2020
  • Sheria ndogo ya kudhibiti Ombaomba inayopendekezwa December 18, 2020
  • MALIPO YA KODI ZA MANISPAA KWA KIPINDI CHA ROBO YA PILI December 10, 2018
  • Angalia Yote

Habari Mpya

  • Rais Magufuli aweka jiwe la msingi ujenzi wa soko la Kisutu

    February 25, 2021
  • Madiwani Ilala wapitisha taarifa ya utendaji kazi kwa kipindi cha Oktoba hadi Disemba, 2020

    February 17, 2021
  • Kamati ya Uchumi na Huduma za Jamii Manispaa ya Ilala yafanya ziara ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo

    February 01, 2021
  • MKUU WA WILAYA YA ILALA AKAGUA MASOKO KATA YA LIWITI

    January 27, 2021
  • Angalia Yote

Video

MANISPAA
Video Zaidi

Kurasa za Karibu

  • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
  • Majengo ya Kihistoria
  • Video za matukio mbalimbali
  • Mradi wa maboresho ya mtaa wa Samora
  • Huduma za kifedha
  • Huduma za Usafirishaji
  • Ratiba ya Mstahiki Meya
  • Ratiba ya Vikao vya Halmashauri
  • Maadili ya Msingi ya Halmashauri

Viunganishi vinavyoelekeana

  • Tovuti ya Ikulu
  • Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora
  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Idara Kuu ya Takwimu
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    1 Mission/Sokoine

    Anuani ya Posta: 20950 Dar es Salaam, Tanzania

    Simu: 2128800

    Simu ya Kiganjani: +255713537815 / +255

    Barua Pepe: info@imc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Siri
    • Kanusho
    • MMM
    • Sitemap
    • Huduma

Copyright ©2017 IMC . All rights reserved.